Dkt. Magufuli atangazwa mshindi Urais Tanzania

0
800

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli kuwa Rais Mteule wa Tanzania.

Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema mgombea huyo amepata kura nyingi halali kuliko mgombea mwingine yeyote.

Akitangaza matokeo hayo, Jaji Kaijage amesema

Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura 29,754,699

Idadi ya waliopiga kura 15,09,950

Kura halali 14,83195

Kura zilizokataliwa 261,755

Kati ya kura hizo, Dkt. John Magufuli (CCM) amepata jumla ya kura 12,516,252 huku mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu akipata kura Tundu Lissu 1,933,271.

Kufuatia ushindi wa Dkt. Magufuli, Jaji Kaijage amemtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania kupitia CCM.