Mwili wa aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa habari wa TBC, Elisha Elia unaagwa leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Segerea Mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tukuyu mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho, Oktoba 27, 2020.
Elisha lifariki dunia Oktoba 24, 2020 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Hapa chini ni taarifa za matukio mbalimbali katika ibada ya kuuaga mwili huo.