Changamoto 5 za Muungano wa Tanzania zilizopatiwa ufumbuzi

0
468

Makamu wa Rais waTanzania, Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao cha kusainiwa kwa hati za makubaliano ya kuondoa changamoto tano za Muungano wa Tanzania zilizopatiwa ufumbuzi.

Sikizila hapa chini kuzifahamu changamoto zilizopatiwa ufumbuzi;

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa hati za kuondoa changamoto hizo, Makamu wa Rais amesema kwamba uwepo wa changamoto haumaanishi kuwa Muungano ni mbovu, kwani hata kwenye familia kuna migongano na njia ya kumaliza ni kupatiwa ufumbuzi.

Aidha, ameagiza changamoto nyingine sita ambazo bado hazijapatiwa ufumbuzi zijadiliwe na suluhisho lipatikane ili muungano huo uendelee kuimarika.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Muungano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) huenda ukawa ndio muungano pekee wa hiyari uliosalia duniani.

Amesema muungano wa nchi nyingine imetokana na vita au nchi mmoja kutawaliwa na nyingine.