Makamu wa Rais Zanzibar azungumzia umuhimu wa hati za makubaliano

0
268

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Seif Ali Idd amesema kusainiwa hati za makubaliano ya kuondoa hoja tano za Muungano wa Tanzania zilizopatiwa ufumbuzi ni kuweka kumbukumbu nzuri pamoja na kurasimisha waliyokubaliana.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Balozi Idd amesema hatua hiyo muhimu katika kuimarisha muungano ni kielelezo tosha kuwa serikali ipo na inafanya kazi yake.

Aidha, ameongeza kuwa kukamilika kwa zoezi hilo “kutasaidia kuwajengea imani wananchi juu ya serikali zao.”

Hafla ya kusainiwa kwa hati hizo imeongozwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.