Rwanda yahalalisha kilimo cha bangi

0
398

Serikali wa Rwanda imehalalisha kilimo cha bangi kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi ikiwa ni njia ya kuongeza mapato ya serikali.

Uamuzi huo ulipitishwa Oktoba 12 mwaka huu katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais Paul Kagame.

Waziri wa afya wa Rwanda, Dkt. Daniel Ngamije amesema licha ya fursa hiyo, matumizi ya dawa hiyo ya kulevya yanaendelea kuzuiwa, na hatua kali zitachukuliwa dhidi watakaokiuka sheria hiyo.

Kwa mujibu wa sheria za Rwanda, matumizi ya dawa hizo hayaruhusiwi hata kwa ajili ya matibabu ambapo daktari atakayemuandikia mgonjwa kutumia bangi kama dawa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na faini takribani milioni 7.