DKT. Magufuli awaomba Watanzania kuiombea Kenya

0
313

Mgombe wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM amewaomba Watanzania kuungana na Wakenya katika maombi ya kuombea taifa hilo dhidi ya Corona.

“Kabla sijajaja kwenye mkutano huu nilikuwa naongea na mwenzangu na rafiki yetu Muheshimiwa Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya, Ameamua nae katika kipindi cha siku tatu kwanzia leo, kesho na jumapili kumwomba ,Mungu ili ugonjwa Corona uondoke Kenya.

“Nawaomba ndugu zangu Watanzania tushirikiane katika maombi haya na wenzetu Wakenya ili ugonjwa wa Corona pia Kenya uondoke kama alivyouondoa Mungu hapa Tanzania,” amesema Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ametoa ombi hilo kabla yakutoa hutuba yake ya kampeni za Urais CCM katika Uwanja wa Mkapa leo.