Wanafunzi zaidi ya 118 wa shule ya Sekondari Oljoro namba 5 wilayani Simanjiro mkoani Manyara wamenusurika Kifo baada ya bweni lao kuungua moto.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa bweni hilo mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti amesema, tukio hilo limetokea wakati wanafunzi wakiwa madarasani na bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo ambalo limeteketeza bweni la wasichana na kuharibu mali zote za wanafunzi yakiwemo magodoro.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Yefred Muyenzi amesema tayari kama serikali ya wilaya wameanza kuchukua hatua za awali ikiwemo kununua Magodoro 100 na vifaa vingine kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi walioathirika.