Kamati ya Maadili ya Kitaifa iliyo chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemsimamisha kuendelea na kampeni kwa muda wa siku saba mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kufuatia madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi katika mikutano ya kampeni inayoendelea hivi sasa.
Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es salaam na Katibu wa Kamati hiyo Emmanuel kavishe na kuongeza kuwa utekelezaji wa amri hiyo unaanza hapo kesho.