Wanachama 20 wa CHADEMA wajiunga CCM

0
749

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewapokea wanachama 20 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wameamua kurudi CCM.

Wanachama hao wameongozwa na Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera, Francis Mutachunzibwa ambaye pia alimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA, Getrude Ndibalema ambaye alijiuzulu uongozi tangu mwaka jana.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mutachunzibwa amesema, “ninaijua vizuri CHADEMA, nilipotea, nilitenda dhambi lakini sasa nimeamua kurudi nyumbani, nipokeeni.

“Ninawaomba wana-Bukoba tumchague Dkt. Magufuli, mashine ya kusaga na kukoboa, jembe la nguvu. Kuanzia kesho, nitamnadi yeye na Advocate Byabato hadi kieleweke.”

Ameongeza kuwa nchi inataka kiongozi mwenye hofu ya Mungu na ili umpate ni lazima watu wajue historia yake. “Kuongoza nchi si lelemama, kiongozi wa nchi ni Mkuu wa Nchi, tena ni Mkuu wa Majeshi.”