JPM: Tupo imara kuendeleza miradi

0
406

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi – (CCM) Dkt. John Magufuli amesema endapo chama hicho kitashinda katika uchaguzi mkuu ujao na kupata ridhaa ya kuongoza, kitaendelea kutekeleza miradi ya kijamii ikiwemo afya, maji, elimu na barabara ili kuboresha maisha ya wananchi.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa akiwa njiani kuelekea mkoani Mbeya katika mwendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Aidha mgombea huyo wa urais amewanadi wagombea ubunge na udiwani huku akisisitiza kuwa wagombea hao watasaidia kuleta maendeleo ya wananchi katika maeneo husika.