Said Mabera wa Msondo Ngoma afariki dunia

0
521

Gwiji wa ukung’utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.

Mtoto wa marehemu, Mabera Said ameiambia TBC kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.