Soko Kuu la Morogoro kuneemesha wafanyabiashara zaidi ya 2000

0
777

Moja ya miradi ya kimkakati ya serikali ni Soko Kuu la mkoa wa Morogoro, soko hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 17, limekamilika na linatarajiwa kufunguliwa Oktoba Mosi, mwaka huu.

Soko hilo lina vikazi zaidi ya 2,000 vya biashara, maduka, huduma za kifedha na sehemu za mazoezi.