RC Shigella atoa Siku 30 kukamilika kwa mradi wa maji

0
253

Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella, ametoa siku 30 kwa watendaji wa mamlaka za maji mkoa wa Tanga kukamilisha zoezi la upatikanaji wa maji katika mradi wa maji Safi kwenye kijiji cha Horohoro kilichopo wilayani Mkinga.

Shigella ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea chanzo hicho kilichogarimu zaidi ya sh milion 360.

Mradi huo ulioanza rasmi mwezi August 2019,mpaka sasa umefikia asilimia 95 huku kiasi cha fedha kilichotumika kikiwa ni zaidi ya sh milion 225.

Zaidi ya wananchi 160, wanatarajia kunufaika na mradi huo ambao mpaka sasa umekwishaanza kutoa maji.