Mgombea wa SAU aahidi ajira kwa Watanzania wote

0
357

Mgombea wa urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingoza Tanzania, atahakikisha kila Mtanzania anapata ajira ya uhakika.

Akizindua kampeni zake katika eneo la kituo cha mabasi Mombasa jijini Dar es Salaam, Mgaywa amesema sera za chama hicho kimejikita katika kutatua kero za wananchi hususani ukosefu wa ajira.

Aidha, ameongeza kuwa iwapo atachaguliwa ataendeleza kazi nzuri iliyofanywa na marais waliopita hususani awamu ya tano kwa kuongeza ndege hadi kufikia hamsini kwa maslahi ya taifa.

Kuhusu suala la aridhi na Maywa amesema kila Mtanzania atamiliki ardhi bila gharama yoyote.

Kwa upande wake mgombea mwenza wa chama hicho, Satia Musa Bebwa amewahakikishia vijana wanaomaliza elimu ya juu kupata mitaji itakayowawezesha kuingiza kipato.

Chama hicho kitaendelea na kampeni zake kesho katika Jimbo la Ubungo na baadaye kuelekea katika mikoa mingine.