CCM: Puuzeni upotoshaji unaofanywa na wagombea wa upinzani

0
450

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya tathmini ya mwenendo wa kampeni zake za uchaguzi mkuu, na kimewashauri wananchi kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ameeleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Geita, na kusema siasa za upotoshaji wa umma si utamaduni wa kitanzania.

Aidha, Polepole amesema CCM imewafanyia wananchi mambo mengi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, huduma za afya, elimu, usafiri wa anga, na itaendelea kutekeleza ahadi zote inazotoa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Katika mkutano huo, mwenezi huyo amesema CCM itahakikisha inapita kila pembe za nchi na kueleza mazuri yaliyofanywa miaka mitano iliyopita, na yale yaliyopangwa kufanyika miaka mitano ijayo.