Waliokimbia Makazi yao Sudan warejea

0
229

Watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko nchini Sudan, wameanza kujerea, licha ya kwamba baadhi ya nyumba zimeharibiwa vibaya na hazifai tena kuwa makazi ya watu.

Mafuriko hayo tayari yamesababisha vifo vya watu 110 huku wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo. Habari zinasema kina cha mto Nile kimeongezeka na maji yameendelea kusambaa katika maeneo ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa.

Baadhi ya watu nchini Sudan ambao nyumba zao zimeharibiwa na mafuriko hayo wanasema walilazimika kukimbilia kwa majirani zao kutafuta hifadhi, lakini baada ya muda wakajikuta tena wamezingirwa na maji.

Watu hao wanasema wanalazimika kusaidiana kama jamii, kwani katika maisha yao yote wamezoea kuishi kama ndugu na majirani zao na kusaidiana.