NEC yarejesha wagombea 15 waliokatwa

0
219

Tume ya Taifa ya Uchaguzi – NEC imetoa uamuzi wa rufaa 55 za Wagombea mbalimbali wa nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, ambapo rufaa 15 kati hizo zimekubaliwa na wagombea kurejeshwa kwenye orodha ya wagombea.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt  Wilson Mahera imeeleza kuwa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa zimekataliwa na rufaa nyingine 25 za kupinga walioteuliwa zimekataliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, NEC imefikia uamuzi huo baada ya kupitia vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa vilivyowasilishwa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa  hizo kuanzia leo na kuendelea,  na kwamba tayari wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kuhusu uamuzi huo.