Dkt. Magufuli afichua sababu ya CCM kutomteua Lugola kugombea Ubunge

0
1240

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa chama hicho hakikumteua Kangi Lugola kugombea ubunge Jimbo la Mwibara baada ya kufungana kura 173 na Charles Kajege, kwa sababu Lugola alijipigia kura moja.

Akizungumza na wakazi wa Bunda mkoani Mara, Magufuli ambaye ni mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho amesema kuwa baada ya wagombea hao kufungana, waliangana nani ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya CCM, ndipo wakabaini Lugola ni mjumbe, hivyo kura moja kati ya kura 173 alizopata alijipigia. Kwa maana hiyo, ukitoa kura aliyojipigia, anabakiwa na kura 172, huku Kajege ambaye si mjumbe akiwa na kura 173.

Msikilize hapa chini akizungumza na wananchi hao;