Mgombea wa CCM, Dkt. Magufuli aahidi neema zaidi Singida

0
289

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli amesema shilingi bilioni 470.4 zimetumika katika miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Singida katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya wakazi wa Singida kumchagua tena katika nafasi ya Urais, Dkt. Magufuli ameainisha miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya 15, hospitali za wilaya tatu, na wakina mama 730 wamefanyiwa upasuaji kupitia hospitali hizo.

Dkt. Magufuli amesema shilingi bilioni 52.6 zimetumika katika ujenzi wa shule, madarasa, mabweni na ukarabati wa shule kongwe za Mwenge na Tumaini

Ameongeza kuwa vijiji 232 vimepata umeme katika mkoa wa Singida na ameahidi kufikisha umeme katika vijiji vyote vilivyosalia katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu.

Mgombea huyo amefanya kampeni katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Manyoni, Ikungi na Singida katika mkoani Singida.