Wananchi Bahi wamngoja Dkt. Magufuli barabarani

0
249

Katika uwanja vya Bahi sokoni jijini Dodoma wakazi tayari wamefurika wakimsubiri mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli.

Baadhi ya wakazi hao wamesema wanakiu kusikia sera za mgombea huyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano iliyokwisha.

Aidha, wamemshukuru Dkt. Magufuli kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya na miradi mbalimbali ya afya na elimu ikiwemo utoaji wa elimu bure ambayo wanasema imesaidia watoto wengi kujiunga na masomo katika wilaya hiyo.