Msanii wa Bongo Muvi, Dude, apata ajali

0
607

Msanii wa Filamu Tanzania, Kulwa Kikumba maarufu Dude amepelekwa Hosptali ya Magomeni jijini Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya Bodaboda kwa kugongwa na gari la kubeba wagonjwa (Ambulance).

Katibu wa wasanii wa Filamu, Jafari Makatu ameeleza kuwa, Dude alikuwa anawahi gari la wasanii ambao wanasafari ya kwenda Dodoma, alivyofika Magomeni Usalama akapata ajali iliyomsababishia majeraha sehemu ya kichwani.

“Alikuwa kwenye bodaboda akagongwa na ambulance. Yeye na dereva wake wote wapo hospitali, amepata majeraha kichwani kwa hiyo ametoka kupiga Xray tunasikilizia majibu kama itashindikana tutamuhamishia Hospitali ya Rufaa wasanii wenzake wote wapo hapa hospitali.

“Mwanzo alikuwa hawezi hata kuongea ila sasa hivi anaendelea vizuri kidogo” amesema Makatu.