Rais wa Mali amejiuzulu na kuvunja Bunge

0
201

Rais wa Mali Ibrahim Keïta ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya wanajeshi waasi kumkamata yeye pamoja na Waziri Mkuu, Boubou Cisse katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako

Rais Keïta pia amelivunja Bunge na kusema “sitaki damu imwagike kisa mimi kubaki madarakani.”

Rais Keïta ametangaza uamuzi huo kupitia Televisheni ya Taifa, na jeshi limetangaza kuunda serikali ya mpito.