Serikali ya Afrika Kusini imeanza kulegeza masharti iliyokuwa imewawekea wakazi wa nchi hiyo ili kukabiliana na virusi hatari vya Corona, vilivyosababisha maafa.
Nchi hiyo hivi sasa imeanza kuridhia uuzwaji wa bidhaa za pombe na sigara ambazo awali ilitangaza kuzifunga ili kuepusha mikusanyiko ya watu iliyokuwa ikisaidia kusambaa kwa haraka kwa Virusi vya Corona.
Nchi hiyo pia imeridhia shughuli za migahawa, hoteli, maeneo ya sterehehe kama baa kufunguliwa, ili kutoa mwanya kwa sekta ya utalii kuendelea kutoa ajira kwa watu mbalimbali wanaotegemea sekta hiyo kujipatia kipata.
Biashara za hoteli na baa ambazo ni maarufu nchini humo, kwa muda mrefu zililikuwa zimefungwa tangu Corona ilipozuka nchini humo, biashara ambayo pia ilikuwa ikichangia katika pato la taifa.