Idara ya Chakula na dawa nchini Marekani imetoa ridhaa kwa wataalamu wa afya nchini humo kuanza kutumia mate kupima kama mtu ameambukizwa virusi vya Corona.
Wizara hiyo imetoa ridhaa hiyo baada ya kuridhika na vipimo vya majaribio vilivyofanywa kwa kutumia mate na kubainika kuwa vipimo vyake viko sahihi.
Vipimo hivyo vitatumika kwa wachezaji wa mchezo wa kikapu na kwa baadhi ya wanafunzi wanaohitaji majibu ya haraka ili kubainika kama wana virusi vya Corona au la.