Afghanistan yaanza kuwaachia wafungwa wa Taliban

0
290

Serikali nchini Afghanistan imeanza kuwaachia wafungwa 400 wa Kundi la Taliban baada ya mazungumzo ya siku tatu ya baraza la viongozi.

Wafungwa hao walikuwa wamefungwa kwa kuhusika na makosa ya mauaji, utekaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni jitihada za kufufua mazungumzo ya amani na kundi hilo la Taliban yaliyokwama kwa muda mrefu.