Idd Nado asaini mkataba mpya AZAM FC

0
193

Winga wa Azam FC, Idd Seleman ‘Nado,’ leo Alhamisi ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja zaidi kuendelea kusalia kwenye timu hii.

Nyongeza hiyo ya mkataba inamfanya kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2022.

Nado amekuwa na kiwango kizuri tokea asajiliwe na timu hiyo msimu uliopita, akifanikiwa kufunga mabao tisa kwenye mashindano yote, saba katika ligi na mawili (Kagame Cup 2019, Rwanda).