India yashika nafasi ya tatu kwa nchi zenye idadi kubwa ya COVID-19

0
309

Ugonjwa wa Corona umeendelea kuathiri baadhi ya mataifa ambapo nchini India takribani watu elfu 67 wamebainika kuwa na virusi vya corona katika kipindi cha siku moja.

Kufuatia maambukizi hayo mapya zaidi ya watu milioni 2.4 wameripotiwa na virusi vya corona nchini humo hadi sasa.

India inakuwa nchi ya tatu kwa idadi kubwa ya watu walioripotiwa kuambukizwa virusi vya Covid – 19 baada ya Marekani na Brazil.

Aidha, kutokana na athari za Corona kampuni kubwa ya usafirishaji duniani ya TUI inasema imepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani katika kipindi cha mwezi Machi hadi Juni.