Tundu Lissu mgombea Urais CHADEMA

0
366

Baraza Kuu la CHADEMA limepitisha Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

Lissu amechukua nafasi hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wanasiasa kadhaa ndani ya chama hicho akiwemo Lazaro Nyalandu na Dkt. Maryrose Majige.

Aidha, akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa wanaangalia uwezekano wa kushirikiana na chama kingine cha upinzani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Mbowe amesema hayo na kubainisha kuwa wanaendelea na mazungumzo na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uwezo wa kushirikiana, huku akiwataka wanachama wa chama hicho kutodharau chama chochote.