Kanisa Katoliki la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Parokia ya Lupaso ambalo ndilo Marehemu Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alikuwa akisali awapo Lupaso.
William Mkapa ambaye ni baba mzazi wa Benjamin Mkapa alikuwa Katekista katika kanisa hili lililoanza kutumika mwaka 1939, na kutabarukiwa mwaka 1947.
Mwaka 2014 Rais Mkapa aliongoza sherehe ya Jubilee ya Miaka 75 ya kanisa hili tangu kuanza kutumika kwake.