Maandalizi ya mazishi ya Rais mstaafu, Mkapa yanavyoendelea Lupaso

0
214

Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, ameeleza hali ya maandalizi ya mazishi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye atazikwa kijiji cha Lupaso, wilayani humo ilivyo.

Akizungumza na TBC, Selemani Mzee ameonesha eneo atakapozikwa Mzee Mkapa ambalo alilichagua kabla ya kufariki dunia.

Akizungumzia namna walivyopokea taarifa, amesema wakazi wa eneo hilo wamehuzunika kwani mbali na kumpoteza kiongozi wa nchi wamempoteza mwanakijiji mwenzao aliyekuwa na mchango mkubwa.