Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Pwani limekamata gari lenye namba T666CSC likiwa limebeba malighafi za chuma chakavu zaidi ya tani kumi likitokea jijini Mbeya kuelekea katika kiwanda cha youn stee kilichopo Kibaha mkoani Pwani bila kibali cha kusafirishia vyuma hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa (NEMC) kanda ya mashariki bwana Arnold Mapinduzi amesema kibali cha kusafirisha vyuma chakavu kinatolewa na waziri mwenye dhamana ya mazingira.
Mapema waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Azan Zungu baada ya kufika kituo cha polisi oysterbay ambapo gari hiyo imeifadhiwa ameagiza nemc kufuata sheria zote zinazotakiwa.
Aidha Zungu ametembelea kiwanda cha youn steer ambacho vyuma hivyo vilikuwa vikipelekwa kibaha mkoani Pwani na kutoa rai kwa wenye magari kubeba mizigo abayo imefuata taratibu zote za vibali.