Shule ya Sekondari Kinondoni Muslim yateketea kwa moto

0
406

Madarasa 11 kati ya 15 ya Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim iliyoko Kinondoni Shamba jijini Dar es Salaam yameteketea kwa moto.

Mbali ya majengo hayo vifaa na samani za shule hiyo vimeteketea kwa moto huku walimu na wanafunzi wote wa shule hiyo wapatao 218 wakisalimika.

Moto huo ulianza majira ya alasiri wakati shughuli za kila siku zikiendelea.

Maafisa wa Jeshi la Zimamoto wamesema ni muhimu maeneo yote ya shule yakawa na maji ya dharura ili kujikinga na madhara ya moto.