Uchaguzi Mkuu: Mbivu na mbichi za CCM kuanza kutengwa leo

0
384

Mchakato wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kupata wagombea katika nafasi mbalimbali unaanza leo ambapo mikutano ya ngazi ya wilaya/majimbo itapiga kura za mapendekezo kati ya leo na kesho.

Upigaji wa kura unaoanza leo unahusisha kura za maoni za kuwapata wagombea katika nafasi za ubunge, uwakilishi, udiwani (Tanzania Bara) na usheha kwenye wadi visiwani Zanzibar.

Baada ya mikutano hiyo, Julai 30 kutakuwa na vikao vya kamati za siasa za majimbo kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo kwenye kamati za siasa za wilaya.

Vikao vya uteuzi kwa wagombea ubunge vitafanywa na Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kwa Tanzania Bara na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ni Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.

Upigaji kura huo unafanyika ikiwa watia nia wa nafasi za ubunge zaidi ya 8,000 wamechukua fomu za kuanzia Julai 14.