Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akionesha fomu ya kuwania kuteuliwa kugombe ubunge Jimbo la Buhigwe Mkoa wa Kigoma kupitia CCM. Mbunge anayemaliza muda wake wa jimbo hilo ni Albert Obama wa CCM.

Waziri wa Uwekezaji, Angellah Kairuki amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Same Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi. Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Same, Victoria Mahembe.

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM. Dkt.Tulia amechukua fomu hiyo leo katika Ofisi za CCM Wilaya akisindikizwa na mume wake, James Mwainyekule.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, leo amechukua fomu za kuomba ateuliwe kugombea ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, kupitia Chama cha Mapinduzi.




