Mtanzania achaguliwa kuwa Balozi wa Universal Music Group Afrika Masharaki

0
616

Sallam SK ambaye ni Meneja wa mwanamuziki amechaguliwa na kampuni inayosimamia wasanii mbalimbali duniani kuwa balozi wake Afrika Mashariki hatua inayotazamiwa kusaidia kukuza muziki wa ukanda huu.

Hayo yameelezwa na mwanamuziki Diamond Platnumz wakati lebo ya WCB ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Usiku wa Zuchu utakao kuwa Julai 18 mwaka huu Mlimani City Dar es Salaam.

“Sijui kama nilitakiwa kusema hili au la, lakini bosi wangu, Sallam, atakuwa Balozi wa Universal Music Group East Africa [Afrika Mashariki], na tunaamini kupitia yeye ataboresha zaidi,” ametangaza Diamond.

Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kufahamu uzoefu alioupata kwa kufanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka minne, na nini kinasababisha wasanii wengine kuilalamikia kampuni hiyo.

Akijibu amesema kuwa amejifunza mengi na kwa kiasi fulani amefanikiwa japo baadhi ya mambo hayakwenda kama walivyotarajia. Ameongeza kuwa uzoefu alioupata utamsaidia endapo ataingia mkataba tena na kampuni hiyo au kama msanii yeyote kutoka WCB ataingia mkataba, kwa sasa ataweza kuwashauri.

Aidha amewashauri wasanii wenzake kwanza wajijengee mizizi ndani ya nchi kabla ya kufanya kazi na kampuni za nje kwani hizo hazina kujuana na pia wawe makini katika mikataba wanayoingia ili wasije wakaishia kupata hasara.

Anaweza kutazama mkutano wao na waandishi wa habari hapa chini;