Masoko ya madini yaongeza mapato sekta ya madini

0
461

Tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini mwezi Machi 2019 mpaka Mei 2020 makusanyo ya mapato ya Serikali yatokanyo na uchimbaji mdogo wa madini yameongezeka hadi kufikia shiligi bilioni 102.44 ukilinganisha na shilingi bilioni 16.23 zilizokusanywa kuanzia Machi 2018 hadi Februari 2019.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Profesa Shukurani Manya wakati alipokuwa akizungumza na Bilionea wa madini ya Tanzanite, Saniniu Laizer katika Maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Profesa Manya amesema matokeo ya ongezeko la mapato katika sekta ya madini ni juhudi za serikali baada ya kufanya udhibiti katika kwa kujenga ukuta wa Mererani, kuwarasimisha wachimbaji wadogo na kuanzisha masoko ya Madini.

Kwa upande wake Bilionea Laizer ameishukuru Serikali kwa kutengeneza mifumo bora na utaratibu mzuri kwa wachimbaji wa madini ambao unawanufaisha wachimbaji wadogo na hata serikali kupata mapato yake stahiki.

Udhibiti wa madini kupitia ujenzi wa ukuta eneo la Mererani umefanikisha kuongeza mapato kufikia shilingi bilioni 2.15 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 92.3 kutoka shilingi milioni 166 Mwaka 2017.