Halmashauri Kuu ya CCM yampitisha kwa kishindo Rais Magufuli

0
286

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika jijini Dodoma, kimepitisha jina la mgombea Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Rais John Magufuli ambalo litapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa utakaoanza hapo kesho jijini Dodoma.

Jina la Rais Magufuli limepelekwa kwenye kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM baada ya kupendekezwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika hapo jana.

CCM ilitangaza mchakato wa kuchukua fomu kwa wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar kuanzia June 15 hadi 30 mwaka huu.

Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Magufuli ndiye mgombea pekee aliyechukua fomu na kwa upande wa Zanzibar walijitokeza Wanachama 32 na waliorejesha fomu ni 31.