Mwenyekiti wa CCM ataka kuchaguliwa kwa mgombea atakayehimili ushindani

0
202

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli ametoa wito kwa wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinachoendelea jijini Dodoma kuchagua mgombea ambaye wanaamini ataenda kushindana na wagombea kutoka vyama vingine vya siasa katika kinyang’anyiro cha Urais Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Rais Magufuli ameyasema hayo jijini Dodoma kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura ili kumpata mgombea mmoja atakayeenda kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar.

Majina yaliyopigiwa kura ili kupata jina moja ni ya Dkt Khalid Salim Mohamed, Dkt Hussein Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha.

Majina hayo ni kati ya majina matano yaliyochujwa ambayo ni Hamisi Musa Omar, Profesa Makame Mbarawa, Dkt Khalid Salim Mohamed, Dkt Hussein Mwinyi na Shamsi Vuai Nahodha.