Rais John Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa viongozi wa jeshi la polisi na usalama wilayani Arumeru mkoani Arusha kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
Akizungumza wakati wa kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Rais Magufuli amesema kuwa viongozi hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kukabiliana na dawa za kulevya, hadi maofisa kutoka makao makuu walipofika na kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha bangi.
Akizungumza wakati wa kuteketeza dawa za kulevya aina ya bangi zilizokamatwa wilayani humo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, James Kaji alisema kuwa mamlaka hiyo itaendelea kukabiliana na dawa za aina yote.
