Maporomoko ya udongo yaua watu 34 Japan  

0
225

 Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko ya udongo pamoja na mafuriko yaliyoikumba Japan hivi karibuni imefikia 34, huku wengine kadhaa wakiwa hawajulikani walipo.

Idadi kubwa ya watu waliokufa katika tukio hilo ni wale waliokuwa wakihifadhiwa katika kituo kimoja cha kulea wazee.

Miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo yaliyokuwa yakiambatana na maporomoko ya udongo pamoja na mvua za msimu ni Kumamoto na Nagoshima.