Rais John Magufuli amemteua Albinus Mgonya kuwa mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Kabla ya uteuzi huo Mgonya alikuwa Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Rukwa na anachukua nafasi ya Mohamed Utaly.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Waziri Kombo kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
Kabla ya uteuzi huo Kombo alikuwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Morogoro na amechukua nafasi ya Wendi Ng’ahala.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza hii leo na wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma hapo kesho saa nne asubuhi.
