SHIRIKA la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo
Barani Afrika (WilDAF) limesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia marekebisho
ya sheria mirathi ili kuweza kutoa haki kwa wajane pindi wanapokuwa
wamefungua shauri linalohusiana na mirathi.
Akizungumza na TBC kuelekea kilele cha siku wajane Duniani Mwanasheria wa
Sherika hilo Zakia Msangi amesema kuwa serikali imekuwa karibu katika
kuhakikisha maboresho ya sheria ya mirathi kwa wajane inaboreshwa na kazi
hiyo wameendelea kuifanya kuweza kupata maboresho hayo.
Amesema kumekuwa na majadiliano ya wadau
mbalimbali wanaoagazia masuala ya sheria ya wajane ,watoto ambapo
serikali imekuwa ikishiriki kwa kuchukua mawazo katika kuweza kufanya maboresho
ya sheria hizo.
“Tumeona dhamira ya serikali katika kufanyia
marekebisho sheria ya mirathi hii itatoa haki kwa wajane ambapo ni
tofauti na ilivyo kwa sasa kwani wajane wengi hawajui hata namna ya kuweza
kufungua shauri la mirathi katika mahakama”amesema Msangi.
Ameongeza katika maboresho juu kuwepo kwa adhabu
ya wafujaji mali za marehmu ili kuweza kuwa fundisho kwa wengine wanaokimbilia
mali huku wakiacha wajane wakiteseka.
Nae Mkurugenzi wa Chama cha Wajane Tanzania
(TAWIA) Rose Sarwatt amesema katika maadhimisho hayo kufanya ni mara sita na
kuwa na mwitikio mkubwa wanawake wajane katika kufikisha kilio chao katika
masuala yanayowazunguka.
Amesema kuwa wana ofisi katika kila kanda ambapo
wajane wengi wamekuwa na changamoto katika mirathi kutokana na mila na desturi
ya wanawake kutopewa kipaombele pindi anapoondokewa na mwenza wake.
Mjane Faith Mwansye-Okoyo amaesema amesema
wajane wanapitia katika changamoto kubwa pindi ndugu wa marehemu
wanapofika katika kuhakikisha wanamiliki mali bila kujua hata mahitaji ya
watoto.
Amesema kuwa katika suala muhimu ni kuwa na
Utamaduni wa kuandika wosia kwa pande zote hali ambayo itapunguza dhuruma za
mali za marehemu.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.