TFF yapitisha rungu kwa wachezaji wa Simba na Yanga

0
508

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewafungia wachezaji wawili wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa utovu wa nidhamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya TFF, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Peter Hellar amesema wachezaji waliofungiwa ni Jonas Mkude wa Simba na Bernard Morrison wa Yanga ambao wamefungiwa mechi mbili na kutozwa faini ya 500,000 kila mmoja.

Aidha Hellar amesema mashauri ya Haji Manara na Antio Nugaz yamerudishwa kwa waliyoyafungua kutokana na ushahidi kutojitosheleza.