Waziri Mwakyembe afungua pazia Tuzo za Waandishi wa habari za SADC

0
195

Washiriki na wanachana wa jumuiya ya SADC wanaoandaa mashindano ya Tuzo za waandishi wa Habari za SADC wamekaribishwa kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwa nisehemu ya kuimarisha mahusiano ya jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati akifungua mkutano wa kutafuta washindi wa tuzo za Waandishi wa Habari kwa nchi za SADC

Waziri Mwakyembe ameongoza mkutano huo kwa njia ya mtandao na wajumbe wa kamati ya kutafuta washindi wa Tuzo za waandishi wa Habari za SADC ambapo Tanzania ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa washindi wa Tuzo hizo watakabidhiwa zawadi zao wakati wa Makabidhiano ya Uenyekiti wa jumuiya ya SADC katika nchi ya Msumbiji mwezi Agosti mwaka huu.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wizara ya Habari Dkt. Hassan Abass ametaja kada zinazoshindaniwa ikiwa ni kutoka kwenye Televisheni, Redio na Magazeti.

Tanzania ni nchi mwenyekiti wa jumuiya ya wanachama SADC chini ya Rais Dkt John Magufuli anayemaliza muda wake mwezi Agosti na kukabidhi kwa Rais wa Msumbiji.