Walimu waaswa kutorubuniwa na wanasiasa

0
291

Waalimu nchini wametahadharishwa kutokubali kurubuniwa na wanasiasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba mwaka huu, na badala yake wameaswa kujikita katika masuala ya kitaaluma.

Tahadhari hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu alipozungumza na zaidi ya walimu 500 jijini Mwanza wanaohudhuria mafunzo endelevu ya elimu ya waalimu.

Katika kuboresha kiwango cha elimu nchini, Serikalil kupitia Taasisi ya Elimu (TEA), imeandaa mtaala mpya wa elimu lengo likiwa ni kuwawezesha walimu wa shule za msingi kuanza kusoma stashahada ya ualimu badala ya cheti kuanzia Julai mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEA, Dkt, Aneth Komba amesema utekelezaji wa mpango huo utaanza na waalimu tarajali.