Kampuni ya Upakuaji Mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi milioni 182, ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika sekta ya afya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada huo kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Mkurugenzi wa Uendeshaji Donald Talawa amesema kuwa TICTS ni sehemu ya watanzania, hivyo inawajibu wa kuunga mkono Serikali katika nyanja mbalimbali.
Talawa amesema kutokana na Serikali kuongeza vituo vya afya, kampuni hiyo imeona kuna umuhimu wa kusaidia vifaa mbalimbali vitavyosaidia vituo vya afya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Talawa ametaja vifaa hivyo walivyokabidhi kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni vitanda 100 ,mashuka, mito, vitakasa mikono ambavyo serikali itapeleka katika vituo vya afya.