Spika wa Bunge, – Job Ndugai amewapongeza Wabunge wa bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalofungwa hii leo kwa kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi.
Spika Ndugai ametoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma wakati akimkaribisha Rais John Magufuli kufunga bunge hilo baada ya kuhitimisha shughuli zake.
Spika Ndugai ametoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma wakati akimkaribisha Rais John Magufuli kufunga bunge hilo baada ya kuhitimisha shughuli zake.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano cha bunge hilo, limeweza kupitisha miswada sitini kuwa sheria, limepitisha maazimio 38, limeuliza maswali ya msingi 3, 376 ambayo yamejibiwa na serikali pamoja na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu 172.
Hafla ya kufungwa kwa bunge hilo la 11 inahudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Rais mstaafu wa awamu wa pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu mzee Benjamin Mkapa, Raia Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete na baadhi ya Mawaziri Wakuu wastaafu.
Bunge la 11 lilizinduliwa na Rais Magufuli mwezi Novemba mwaka 2015.