VIDEO: Simba yamwagiwa sifa kedekede bungeni

0
766

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekimwagia sifa kikosi cha timu ya Simba cha jijini Dar es salaam kwa kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara na kukaribia kutwaa kwa mara ya tatu ubingwa wa ligi hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa amemwaga sifa hizo bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amekipamba kikosi cha timu ya Simba kwa ubora wa hali ya juu, huku akisisitiza kuwa hakuna timu itakayokizuia kikosi hicho kutwaa taji msimu huu.