Raia 239 wa India waliokwama nchini warejea nchini mwao

0
164

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imewasafirisha kurejea nchini mwao, raia 239 wa India waliokwama nchini baada ya nchi nyingi duniani kufunga anga kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Kurejea nchini India kwa raia hao kumetoka na nchi nyingi duniani kuanza kufungua anga zao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona kuendelea kupungua.

Abiria hao raia wa India wamesafirishwa na ndege ya ATCL namba 707 Dreamliner.

Safari hiyo ni ya pili kwa ndege ya ATCL ikiwa na abiria kutoka nje ya nchi, baada ya kuanza kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona katika nchi mbalimbali duniani.