TFF yapitisha marekebisho ya kanuni

0
596

Shirikisho la Soka nchini (TFF) limepitisha marekebisho ya kanuni ya ongezeko la wachezaji wa kufanyiwa mabadiliko kutoka watatu hadi watano.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kutokana na janga la corona, yataanza kutumika kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayorejea hapo kesho.